NANI MWENYEZI MUNGU

Posted by Unknown


Nani mwenyezi Mungu? 

Unapo sema mwenyezi Mungu
Ni uweza unaoweza usiwezwa na kinacho wezeshwa.
Ambaye si mwingine bali ni yeye muumbaji.
 
2:225 
" mwenyezi Mungu hakuna mola ila yeye..........."
Ni mwenye kuumba na kuanzisha kila jambo
 
2:117 " yeye ndie muumbaji wa mbingu na ardhi na anapo taka jambo huliambia kua likawa"
 
33:6 
zaburi " kwa neno la BWANA mbingu ilifanyika na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa."
 

Ambaye Mwenyezi Mungu ni mwenye kujulikana kwa majina mazuri.
 
Kwa kiswahili una sema Mwenyezi Mungu
Kiarabu Allah.
 
Waingereza wanamwita God.
Lakini kumwita Mwenyezi Mungu kwa jina la God ni kosa sababu Mwenyezi Mungu ni mmoja.
Na neno God lina wingi ambao ni Gods.
 
Na jina Allah halina wingi. 


UISLAM UNAAMINI KITABU GANI

Posted by Unknown



 

Uislam unaamini kitabu gani?

Tunapo ongea kuhusu vitabu vya Mungu. Basi jua kwamba  vitabu vyote ni mali ya waislam. Sababu hakuna kitabu kilishuka kwa kuwaongoza watu nje ya uislam. Na uhalisia ni kwamba kila kitabu kilishuka ili kiwaongoze waislam wa zama hizo.

Qur an 3:3 "aliteremsha taurat na injili zamani ili ziwe uongozi kwa watu"
Vitabu vya Allah ni

1 Taurat
Kitabu hiki kilishuka mlima sinai kupitia nabii Musa.

4:4 malaki " ikumbukeni torati ya musa mtumishi wangu" hapo unaona torati ni ya Musa lakini Musa dini gani?

Zaburi ya daudi jee Daudi dini gani?
1:14 marko injili ya Yesu jee Yesu dini gani?

Qur an Muhammad (saw) jee Muhammad dini gani?
Jibu hawa wote dini yao ni moja

42:13 " amekupeni sharia ya dini ile ile tuliyo muusia Nuhu na tukakufunulia wewe

Na tuka muusia Ibrahim Na Musa Na Issa kwamba simamisheni dini wala msifarikiane kwayo"

Nadhani mpaka hapo tumejua kuwa vitabu hivyo walishushiwa

manabii na manabii hao dini yao ni moja japo walikuja kwa nyakati tofauti.

Jee ipi dini ya manabii???

Na kipi kitabu cha mkiristo?

Mkiristo hana kitabu sababu hana nabii na hakuna nabii Mkiristo.

Usikose mada ipi dini ya manabii.


 

MUNGU NI MMOJA

Posted by Unknown







Mwenyezi Mungu mmoja.
Tunapo sema Mungu mmoja.
Hii ndiyo imani msingi ya uislam.

Kwani hakuna dini inayo amini Mungu mmoja zaidi ya uislam. Na zilizo baki zote ni zile zenye kumshirikisha Mungu kwa kujenga imani ya utatu.
Na hii imani ya Mungu mmoja ni imani yake tangu manabii wa zamani.

20:3 Kutoka " usiwe na miungu mingine ila mimi" haya maneno anaambiwa nabii Musa as.
Kwamba Mungu ni mmoja.

83:18 zaburi " wajue ya kuwa wewe uitwaye jina lako Yehova ndiwe peke yako uliye juu, juu ya nchi yote. Huyu ni nabii Daud anafundisha Mungu mmoja.

17:3 Yohana." Na uzima wa milele ndiyo huu wakujue wewe munguvwa pekee wa kweli na Yesu kristo uliye mtuma." Yesu naye anafundisha kuwa kuna mungu mmoja. Lakini ajabu utashangaa mtu anakwambia eti yesu ndiye Mungu mwenyewe.

Itakuwa ni kichekesho kama si msiba kuamini kuwa yesu ni Mungu.

114:1 qur an " sema yeye ni mwenyezi mungu mmoja tu" mafundisho ya mtume Muhammad sa


Imani ya Mungu ni imani ya uislam.
Sababu imani nje ya uislam haisimami kwa uwepo wa Mungu mmoja ila husimama kwa kumshirikisha Muumba wao na kuamini kuwa Mungu ni watatu. Jambo ambalo uislam haukubali

5:73 qur an " bila shaka wamekufuru wale wanao sema Mwenyezi Mungu ni mmoja katika watatu..............."

Basi tujiepushe na shirki ya kusema mungu ni utatu kwa kusimama katika tauhidi ya kuamini Mungu ni mmoja.