YESU NI NANI?

Posted by Unknown


LEO DUNIA INA VITUKO KILA AINA


inashangaza kusikia kuwa kuna binaadamu wenzetu wanasema kuwa Yesu ni Mungu wao.
8:40 Yohana "lakini sasa mnatafuta kuniua mimi mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli niliyo isikia Mungu."

hii ni kauli ya Yesu huyo ambaye wanaitikadi kuwa ni Mungu, anasema kuwa yeye ni MTU aliye siki maneno toka kwa MUNGU.
Inawezekanaje aliyetumwa na Mungu kuwa MUNGU??
lazima iwe ajabu pia zingatia kuwa
23:19 hesabu "mungu si mtu aseme uongo, wala si mwanaadamu ajute"

lakini Yesu anasema kuwa yeye ni mtu, vipi awe Mungu?
3:16 Yohana  "kwa maana jinsi hii mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele"

hoja

huyo mwana mpendwa aliye tumwa na Mungu ni nani?

kama mwana ni Yesu jee mungu ni nani ili yesu awe mwana??

kama mungu ni yesu jee mwana ni nani ili yesu awe mungu??

ni wazi yesu si mungu
islamicdaawa19.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment